Mwanaharakati wa masuala ya mitandao Carry Mastory amesema kuwa kwa upande wake hajabariki kabisa mahusiano ya msanii wa Bongo Fleva, Whopzu na malkia wa Bongo Movies, Wema Sepetu 'Last Born wa Taifa' kwa kile alichodai kuwa hawaendani.
Akizungumzia uhusiano huo, Carry amedai kuwa Wema amepora Tunda mwanaume wake na kuongeza kwamba Whozu nza mzazi mwenzake, Tunda walikuwa wanaendana lakini Wema aliingilia penzi hilo na kuliharibu.
Aidha, Carry amedai kuwa kwa taarifa alizozipata kutoka kwa watu wa karibu wa Wema, tayari Wema ana ujauzito wa miezi miwili lakini haamini mpaka atakapoona tumbo kwa Wema.
"Mimi Wema namuonea huruma, sababu ndiye binti aliyetakiwa awe na mafanikio, tusimuite binti kwa sababu alitakiwa awe mama, lakini Mwenyezi Mungu hajabariki hilo.
"Tulitamani kumuona Wema kama msanii wa kike mwenye mafanikio kuliko hata akina Irene Uwoya, zaidi ya wasanii wote wa kike, lakini hali yake ndiyo mbaya.
Ukimwangalia Whozu na Tunda wanaendana ‘same age’ ni watu ambao kweli wanastahili kuzaa na kuwa na mtoto.
"Mwanaume aliyeko kwenye ndoa anachukuliwa na mchepuko ambaye ni mdogo, na siyo jimama. Tumeshangaa Wema kuingilia lile penzi na kumchukua kijana mdogo halafu ndiyo anajitapa Chimama, Chibaba, inashangaza sana.
"Za chini chini nimesikia Wema ana ujauzito wa miezi miwili, nakumbuka tulishaabiwa Wema ni mjamzito halafu akatapika matembele, ujauzito na matembele wapi na wapi?
"Kwa hiyo mimi nikisikia stori yoyote ya Wema sasa hivi siamini, mpaka nione, mimba haijifichi, miezi saba au nane tutaona lakini penzi la Wema na Whozu mimi sijalibariki," amesema Carry.