Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Exclusive:Wafunga Ndoa wodini baada ya mume kupata ajali na kukatwa mguu (video+)

Video Archive
Thu, 23 Sep 2021 Chanzo: millardayo.com

Ndoa ya kijana Augustine Makule na mpenzi wake Rose Kimaro imevuta hisia za wengi jijini Dodoma baada ya wawili hao kufunga ndoa wodini. Hatua hiyo imekuja baada ya Bwana harusi kupata ajali ya Bodaboda siku mbili kabla ya siku ya ndoa yao.

Ajali hiyo ya pikipiki iliyotokea eneo la zuzu Dodoma imepelekea kijana Agustino kukatwa mguu wake wa kulia na vidole vitatu vya mguu wake wa kushoto.

Licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo waliamua kuendelea na ratiba yao ya ndoa ambayo waliifungia ndani ya wodi ambapo mchungaji alifika na baadhi ya waumini na kuendelea na taratibu za ndoa.

Chanzo: millardayo.com