Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Exclusive: Mbosso akiri kuzaa na mke wa Abdul Kiba, "alinianza"

MBOSSO NA ABDUL KIBA Mbosso asimulia mwanzo mwisho alivyozaa na mke wa Abdul Kiba

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbosso kutoka pale WCB ametusanua bwana kwamba, aliwahi kuzaa na aliyekuwa mke wa mdogo wake Alikiba, Abdul Kiba.

Mbosso amefunguka hayo kupitia kipindi cha BIG SUNDAY cha Wasafi ambapo msanii huyo aliulizwa maswali mbalimbali likiwemo hilo la kuzaa na aliyekuwa mke wa Addul Kiba.

Awali, Mbosso alianza kwa kusema kuwa aliwahi kufanya jambo hilo lakini ni zamani na kwamba kwa sasa hana tatizo na Abdul.

“Sina tatizo na Abdul Kiba, labda huko zamani ilitokea kwa bahati mbaya kwa sababu tulikuwa hatujui na unajua dada zetu huwa hawasemagi na wao pia sometimes wanataka huku na huku, lakini ni mwanangu na hatuingiliani,” alisema Mbosso.

Alipobanywa zaidi na watangazaji wa kipindi hicho, kwamba aeleze hasa nini kilitokea hadi akajikuta ametembea na aliyekuwa mke wa Abdul Kiba ndipo alipofafanua suala hilo kwa kusema uhusiano wao ulianzia kwenye kununua biriani.

“Kuna siku moja nilikuwa pale mlipokuwa mnafanya Wasafi Village. Nikakutana na misosi misosi kwenye Instagram inauzwa. Nikamtumia oda ya biriani. Nikaweka oda ya biriani, biriani ikaja na pikipiki mpaka Wasafi Village.

“Tukaenda hivyo biriani nikawa nimelielewa. Siku moja huyo muuza biriani akaniandikia meseji unajua mimi shabiki wako? Nikamwambia nashukuru. Nikamwambia mimi lakini sikujui maana naona mabiriani. So mabiriani yakawa mabiriani,” anaeleza Mbosso.

Mbosso anasema muda ulivyozidi kwenda wakiwa tayari wameshabadilishana namba, siku moja mdada huyo akamwambia atamfuata Zanzibar katika shoo yake kumuunga mkono.

“Kweli bwana mtoto akaja nini hatukuonana mapema lakini wakati wa shoo nikiwa jukwaani kama nikamuona hivi alikuwa karibu ya jukwaa na wakati mimi naimba akawa kama ananionesha hivi ndio mimi, tukasomana,” anasimulia.

Anasema baada ya muda, wakaja kukutana tena jijini Dar akiwa maeneo ya Magomeni baada ya mrembo huyo kumualika kwenda kunywa kahawa nyumbani kwake.

“Tulikuwa na wanangu pale basi tukiwa tayari tushafanya mambo mengi naye, ndio Santos (ndugu wa Diamond) akaja pale akatukuta. Kesho yake Santos ndiyo akanisanua kwamba yule bwana ni mke wa mshikaji. Niliumia sana na nikamlaumu sana yule binti kwa nini hakuniambia mapema?

“Sijakaa sawa ndio akaniambia ni mjamzito na ndio ikawa hivyo. Nilimchukia sana sababu nilimwambia alitakiwa aniambie maana mimi na mwana tushakutana sana kwenye mambo hayo hivyo ikawa kama vile tunarudisha tena mabifu wakati wakati huo sisi tulikuwa pisi na mshkaji,” anasimulia Mbosso.

Mbosso alitumia kipindi hicho kumuomba radhi Abdul kama atakuwa amemkosea lakini ni kwamba hakujua hivyo asimuelewe vibaya. Hata hivyo mrembo huyo alishaachana na Abdul Kiba na Mbosso hakuweka wazi kama wanaliendeleza au wamebaki kuwa mtu na mzazi mwenziye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live