Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Exclusive: Jux kufunguka ndoa hivi karibuni

Jux Na Baby.png Exclusive: Jux kufunguka ndoa hivi karibuni

Thu, 4 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo R&B Juma Jux amedokeza kuwa anapanga kufunga ndoa na mpenzi wake hivi karibuni.

Jux ameweka wazi kuwa anaithamini sana ndoa na kubainisha kuwa anakusudia kupiga hatua hiyo.

"Ndoa ni kitu kizuri. Nitafunga ndoa hivi karibuni. Mtajua ikifika," Jux alisema katika mahojiano na waandishi wa habari.

Mpenzi huyo wa zamani wa Vanessa Mdee hata hivyo hakumfichua mchumba wake ambaye anakusudia kuoa.

"Utafika muda mtamjua," Alisema.

Mapema mwaka huu, Jux alidaiwa kuwa kwenye mahusiano na mrembo mmoja kutoka Rwanda anayefahamika kwa jina la Karen. Mrembo huyo aliripotiwa kuwa mpenzi wa mwanamuziki huyo baada ya kuoneka akiendesha Benz lake na hata kutembea kwake usiku.

Malkia huyo hata hivyo alidaiwa kumtema Jux kufuatia uhusiano wake wa kutiliwa shaka na mwasoshalaiti wa Kenya Huddah Monroe.

Katika kipindi cha takriban miezi miwili ambacho kimepita kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Jux ana mahusiano na mrembo kutoka Kenya, Huddah Munroe. Madai kuwa wawili hao kuwa penzini yalivuma zaidi baada ya kuonekana wakibusu hadharani mara kwa mara.

Hata hivyo wasanii hao tayari wamejitokeza kueleza kuwa uhusiano wao ni wa kirafiki ila sio wa kimapenzi.

"Mimi nipo kwenye mahusiano na najua Huddah yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwahiyo swala la sisi wawili kuwa wapenzi halijitokezi. Lakini nitalijibu swali hili siku nyingine. Lolote linaweza kutokea." Jux alisema katika mahusiano ya hapo awali.

Jux aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Vanessa kwa takriban miaka sita lakini mahusiano yao yakagonga mwamba mwaka wa 2019. Miezi kadhaa baadae Vanessa alijitosa kwenye mahusiano na Rotimi kutoka ambaye tayari wana mtoto mmoja pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live