Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Exclusive: Diamond azuiwa kununua ndege binafsi, sababu zatajwa

Diamond Mama Ndege Exclusive: Diamond azuiwa kununua ndege binafsi, sababu zatajwa

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: Global Publishers

Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz; ni supastaa wa muziki wa kimataifa kutoka nchini Tanzania ambaye hivi karibuni alitangaza kununua ndege binafsi, lakini rubani amemzuia kufanya hivyo akianika siri nzito nyuma ya pazia, IJUMAA lina exclusive.

Hayo yanajiri siku kadhaa baada ya uongozi wa Diamond kupitia mmoja wa mameneja wake, Babu Tale kukiri kwamba, tayari kila kitu kimekamilika na ndege hiyo ilipaswa kutua nchini wiki hii.

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, rubani maarufu nchini Tanzania, Kapteni Alia Mndeme ameeleza sababu za Diamond au Mondi kuzuiwa kununua ndege binafsi akieleza hasara za kumiliki usafiri huo.

Kapteni Mndeme anasema kuwa, kikubwa atakachonufaika nacho mtu anayemiliki ndege binafsi ni kupanga mwenyewe muda wake wa safari, lakini anatakiwa kujipanga mno kiuchumi na kama ana njaa ya mafanikio kama ilivyo kwa Diamond au Mondi, hilo siyo jambo la kipaumbele;

IJUMAA: Licha ya kujipanga, anafaidika na nini kwa kuwa na ndege yake?

KAPTENI MNDEME: Kikubwa inakuwa ni urahisi wa safari, anakuwa hapangiwi muda, yeye mwenyewe anapanga muda wake wa safari.

IJUMAA: Lakini kumiliki ndege ni jambo kubwa unamshauri nini Diamond?

KAPTENI MNDEME: Namwambia tu kwamba ni kitu kikubwa kumiliki ndege binafsi, hasa kwa mtu mwenye safari nyingi za mbali, anamiliki muda wake mwenyewe, lakini ajue mwanzoni inakuwa ngumu kwa sababu ya gharama za vibali kama leseni n.k, baada ya hapo vingine vyote ni vyepesi tu.

IJUMAA: Mtu binafsi unapokuwa na ndege, huwa hakuna ugumu katika kuingia au kutoka uwanja wa ndege?

KAPTENI MNDEME: Huwa hakuna tatizo, unaweza kuingia na kutoka katika viwanja vya ndege tofauti vya hapa nchini kwa sababu hiyo ndege inakuwa imesajiliwa kwa hapa Tanzania.

IJUMAA: Diamond anaweza kufanya biashara ya kukodisha ndege? Au Kuna matatizo kufanya hivyo?

KAPTENI MNDEME: Kuhusu uwezekano wa kuikodisha ndege hiyo, ni biashara inayowezekana endapo atapata leseni za kukodisha, lakini pia ataweza kusafiri hadi nje ya nchi, ingawa gharama zake ni kubwa.

IJUMAA: Kwani kumiliki ndege kunahitaji mtaji mkubwa kuiendesha?

KAPTENI MNDEME: Kumiliki ndege ni jambo jema, lakini ni lazima ajipange sana, maana gharama za uendeshaji siyo za kitoto, zipo juu kwa kila kitu, kuanzia umiliki, mafuta, malipo ya wafanyakazi utakaowaajiri na kadhalika.

Ikumbukwe ukiachana na wasanii kama Davido Wizkid, Don Jazzy, DJ Cuppy na wengine, pia wacheza soka wa kulipwa barani Afrika, waliokwenda kukipiga Ulaya kwa mafanikio wengi wao wana ndege binafsi, wakiwamo Samuel Eto’o na Didier Drogba.

Chanzo: Global Publishers