Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ex girlfriend atua mahakamani kudai apewe mali

Israel Picdf.png Ex girlfriend atua mahakamani kudai apewe mali

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mpenzi wa bondia wa ngumi za vizimba, Israel Adesanya mrembo Charlotte Powdrell amefungua mashtaka mahakamani kudai nusu ya mali za bondia huyo akidai wamekuwa kwenye mahusiano naye muda mrefu hivyo ana mchango kwenye safari yake ya mafanikio.

Adesanya ambaye ni bingwa wa uzito wa kati wa Ultimate Fighting Championship (UFC) alipata umaarufu zaidi baada ya kumchapa Alex Pereira kwa KO katika pambano lililomfanya mwimbaji maarufu duniani Drake kushinda Sh6.28 bilioni baada ya kubeti kwamba Adesanya angeshinda.

Ishu ya bondia Adasanya kushtakiwa na mpenzi wake wa zamani iliwekwa wazi na bondia mwenzake, Sean O'Malley, aliyeweka mambo wazi kupitia kipindi kilichokuwa mubashara kwenye chaneli ya YouTube Suga.

Adesanya na mrembo Charlotte hawajafunga ndoa, wala hawana mtoto, lakini mwanamke huyo anaamini anastahili walau nusu ya utajiri wa mwanamume huyo kwa kuwa walikuwa pamoja kwenye uhusiano kwa kipindi anatafuta na kupata mali.

"Sijui mahusiano yao yalikuwaje kwasababu sikujua kama ana mpenzi, ila kutaka nusu ya mali zake ni kitu kinafurahisha," alisema bondia O'Malley.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live