Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eti Mshindi BSS ni wa Mchongo?

Bryson Bss Mshindi wa BSS

Tue, 18 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSHIRIKI kutoka Dar, Brayson Yohana ameibuka Mshindi wa Shindano la 12 la kusaka vipaji (Bongo Star Search – BSS) msimu wa 2021/22 na kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni 20 na zawadi nyingine mbalimbali kutoka kwa wadhamini tofauti ikiwemo ofa ya kuishi bure kwa mwezi mzima kwenye apartment za Palm Village, Mikocheni jijini Dar.

Ushindi huo aliutwaa wikiendi iliyopita jiji Dar, mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Mechezo, Mohammed Mchengerwa.

Tofauti na miaka mingine ambapo minong’ono juu ya mshindi husikika kila kona ikidaiwa mshindi ni wa mchongo, mwaka huu haikuwa hivyo.

Wengi wa waliokuwa wakifuatilia mchakato huo tangu mwanzo wanasema kuwa, amestahili kushika namba moja katika shindano hilo maarufu Tanzania.

Wanasema kuwa, uwezo wake wa kuimba siyo wa nchi hii akiwa na shahada ya muziki kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wanasema kuwa, wale ambao wanasema jamaa huyo amependelewa, wanazingua kwani jamaa ni fundi, anaujua muziki kitaalam na ana kipaji pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live