Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esma afunga ndoa na Jembe One

Jembe One Esma Esma afunga ndoa na Jembe One

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dada yake wa supastaa wa Bongo Felva, Diamond Platnumz aitwaye Esma Platnumz siku ya jana ameozeshwa rasmi kuwa mke halali wa Meneja wa Mwanamuziki Mavokali, Rashid Shaibu maarufu kama Jembe One katika Msikiti wa "Masjid Akram" uliopo Mbezi Beach, Dar Es Salaam.

Ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Masjid Akram Uliopo Mbezi Beach, jijini Dar Es Salaam jioni ya jana Februari 22,2024.



Baada ya msikitini shughuli ilihamia nyumbani na upande wa ukweni shughuli hii ilihudhuriwa na Mama mzazi wa Esma Platnumz, Mama Dangote, kaka wa Esma na Diamond aitwaye Ricardo Momo, Iddy Santos na wengine.

Hii ni ndoa ya tatu kwa Esma ambapo ya kwanza alifunga na mwanamitandao Petit Mani mnamo Septemba 2014 na Julai 2020 alifunga ndoa na mfanyabiashara Yahya Msizwa, baada ya ile na Petit kuvunjika.

Hongera sana Esmap na Jembe One kwa kufunga pingu za maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live