Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esma: Sipo upande wa wifi yeyote

ESMA123 Esma: Sipo upande wa wifi yeyote

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Esma Khan au Esma Platnumz; ni mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii aliyepata umaarufu kupitia kaka yake ambaye ni staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye anasema kuwa, hana wifi ambaye amemchagua wa kuwa upande wake.

Anasema kuwa, hii ni kwa sababu siku ambayo kaka yake (Diamond) atamwambia waanze kuandaa harusi, huyo ndiye anaweza kufungua kinywa na kusema ndiye wifi yake.

Akizungumza na Gazeti la IJMAA, Esma anasema kuwa, suala la kusimama upande wa wifi mmoja ni jambo ambalo tayari lilishathibitishwa na kaka yake kuwa ndiye wifi mwenyewe na harusi iko njiani kama ilivyo kawaida ya maandalizi.

“Mimi mambo ya kuitwa Yuda sitaki kabisa kwani hivi sipo upande wa wifi yeyote na ndiyo maana mtu yeyote nipo naye mpaka hapo mwenyewe Diamond atakapotutambulisha rasmi mtoto wetu na si vinginevyo,” anasema Esma akiwazungumzia wanawake wanaohusishwa kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live