Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esma Ndoa ya Nne Yanukia

ESMA123 ESMA

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HABARI za ndani kabisa zinadai kwamba, ndoa ya nne ya dada wa staa wa muziki Afrika, Diamond Platnumz aitwaye Esma Platnumz, inanukia.

Kwa mujibu wa watu wa Madale; nyumbani kwa Mama Dangote, tayari vikao vinaendelea kwa siri kwa sababu haitakiwi kuwa ndoa ya matangazo kama ilivyokuwa wakati alipoolewa na yule tajiri Msizwa ambapo tukio hilo lilitafuna zaidi ya shilingi milioni 300 za Kitanzania.

Chanzo kimesema ishu hiyo imekuwa ikifanyika kwa siri bila kujulikana Esma anaolewa na nani, lakini wapo wanaojua anayemuoa ni Uchebe; yule aliyekuwa mume wa Shilole.

Kama ni kweli Esma anaolewa, basi itakuwa ni ndoa ya nne baada ya kuolewa na Baba Tahiya, Baba Taraj (Petit Man) na Msizwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live