Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esma, Mama Dangote na skendo ya vibenteni

Esma Na Mama D Mama Dangote na Esma

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya Alhamisi, Februari 2, 2023, dada ya mwimbaji Diamond Platnumz, Esma Khan aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 37 humu duniani.

Katika siku hiyo maalum kwake, mama yake Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote alikiri kujivunia yeye.

Mama Dangote alisema anajivunia kumzaa na kumlea Esma huku akimtakia maisha marefu zaidi.

"Sina chakuandika, ila najivunia kukuzaa na kuwa Mama Bora kwako Esma, Esma Platnumz nakutakia maisha marefu yenye baraka tele kwenye kuongeza mwaka mwingine," aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Katika jibu lake, Esma alimshukuru mzazi huyo wake na kudokeza kuwa ameiga mfano wake katika kuwalea binti zake.

Kama kawaida, wanamitandao wengine pia walitoa maoni kwenye chapisho hilo. Mwanadada mmoja alinasa umakini wa Esma alitilia shaka ukamilifu wake akidai kuwa hangeweza kutulia katika ndoa bali, pamoja na mamake, walijihusisha na wanaume wadogo tu.

"Una ubora gani kila siku unaachika kazi kulea vibenten wewe na mama yako," Lynne Mtandi alimwambia Esma.

Mama huyo wa watoto watatu hakafutilia mbali tetesi za mwanadada huyo bali alijigamba kwa kuweza kufikia hatua ya kuvishwa pete.

"Ndo majaaliwa yangu bora na ninaolewa kuna watu wanaachika bila hata pete kuvishwa kila siku," alijibu Esma.

Mtumizi mwingine wa Instagram alimshtumu Esma kwa kuwa mfano mbaya kwa binti zake kuhusu suala la ndoa.

"Ukweli amekuwa mama Bora lakini hana mfano mzuri ktk mabinti zake mama asiye na Ndoa ni jambo Dogo lakini ni kubwa kwa mafunzo kwa watoto tunachukulia poa lakini sivyo address ina umuhimu sana tena yeye Kazaa mabinti," Nashe Ngena alimwambia.

Kufikia sasa, dada huyo wa Diamond anadaiwa kuondoka kwenye mahusiano kadhaa ikiwemo ndoa mbili halisi.

Ndoa ya mwisho ya Esma aliolewa kama mke wa tatu kwa mfanyabiashara wa Tanzania, Maulid Msizwa mwaka wa 2020 lakini ndoa hiyo ilidumu kwa miezi mitatu pekee. Kwa sasa anadaiwa kuwa kwenye mahusiano mapya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live