Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esma: Harmonize ni mtu wetu na Wasafi inafurahia mafanikio yake

Kajala PaulaWAKALI Esma: Harmonize ni mtu wetu na Wasafi inafurahia mafanikio yake

Sat, 16 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ESMA Khan au Esma Platnumz; ni dada wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye anasema kuwa, hakuna uhasama wowote kati ya kaka huyo na aliyekuwa msanii wake, Harmonize au Konde Boy Mjeshi.

Esma ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) anasema kuwa, mashabiki ndiyo wamekuwa wakitengeneza bifu kati ya wasanii hao wawili ilihali kiuhalisia hanana tatizo. “Ninyi ndiyo mnawagombanisha.

Siyo wao. Wao wako sawa kabisa,” anasema Esma. Mama huyo wa watoto wawili anamtaja Harmonize kama mtoto wa Diamond na kusema kaka’ke hawezi kubishana naye.

Esma anasema kwamba familia ya Wasafi inafurahia mafanikio ya Harmonize kwa kuwa aliwahi kuwa mmojawao.

“Tunatamani kumuona Harmonize akipiga hatua kwa sababu ni mtu wetu, ametoka kwetu. Tunafurahi akiwa anazidi kupiga hatua. Hakuna kinachotuuma kwa kuwa ni mtu wetu. Diamond hawezi kujibizana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live