Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esma: Familia hatuna habari kuhusu Dianond na Zuchu

Mond Na Zuchu Diamond na Zuchu

Sun, 26 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Esma Khan au Esma Platnumz; ni dada wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika akiiwakilisha vyema Nchi ya Tanzania kimataifa, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz ambaye amefunguka mazito juu ya penzi la kaka yake huyo na msanii wake, Zuhura Othman au Zuchu.

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA, Esma ambaye yeye na mama yake, Sanura Kassim au Mama Dangote wanatajwa kuwa waamuzi wa mwisho juu ni mwanamke gani awe na Diamond, anasema kuwa, wao kama familia hawana wanachokijua juu ya penzi hilo;

IJUMAA: Vipi kuhusu Zuchu? Ninamaanisha kuhusu uhusiano wake na Diamond au Mondi?

ESMA: Yaani ukweli sisi (familia) hatuna tunachojua kama kuna uhusiano wa kimapenzi unaoendelea, mimi najua ni mtu na bosi wake tu na si vinginevyo.

IJUMAA: Mbona kama wanaweka wazi sana kwamba ni wapenzi hivi sasa?

ESMA: Hapana, yule ni mtu na bosi wake tu, hakuna uhusiano.

IJUMAA: Na kuhusu Aaliyah (Mtangazaji wa Wasafi TV), maana naona ni marafiki na pia inadaiwa naye ana uhusiano wa kimapenzi na Diamond?

Nini maoni yako baada ya majibu ya Esma?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live