Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esha Buheti Atamani Kumpamba Rais Samia

SAMIA ESHAAA Esha Buheti Atamani Kumpamba Rais Samia

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMAMA mwigizaji wa Bongo Movies na mjasiriamali, Esha Buheti anasema amehitimu mafunzo ya utengenezaji wa keki zitakazokuwa gumzo kwa kuwa atazitengeneza kwa staili ya sura ya mhusika.

Esha amesema kuwa, baada ya mafunzo hayo, sasa anatamani kutengeneza keki itakayokuwa na nakshi zilizopambwa na picha ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Esha anasema kuwa, moja ya ujuzi aliopata katika mafunzo hayo ni upikaji keki kwa kutengeneza picha na maumbo ya vitu mbalimbali.

Anasema ili kupima ujuzi wake, atatengeneza keki maalum atakayoipamba kwa picha ya sura ya Rais Samia na kama itawezekana atampatia kama zawadi.

“Nimepata mafunzo ambayo yameongezea kipaji changu cha kupika, napenda sana kupika ndiyo maana napambana ili niwe mpishi bora mwenye vyakula vilivyoandaliwa kwa ustadi mkubwa,” anasema Esha.

Anaongeza kuwa, licha ya kuwa na ndoto ya kumtengenezea keki Rais, anatamani pia kumnadi mwanamuziki Nasibu Abdul au Diamond Platnumz kwa kuuza keki zenye picha ya sura yake.

Esha amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazopatikana au mafunzo yanayotolewa na wakufunzi wa masuala mbalimbali kwa ajili ya kuongeza ujuzi.

Msanii huyo alikuwa miongoni mwa watu 15 waliopata mafunzo ya siku tano ya upishi wa keki jijini Dar yaliyotolewa na mpishi maarufu aitwaye Tuba Geckil kutoka Uturuki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live