Menu ›
Burudani
Wed, 22 Feb 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi na wenzake 17 wameshtakiwa kwa kosa la kufanya maandamano kinyume cha sheria kwenye viunga vya Jengo la Bunge jana Jijini Nairobi. Hata hivyo Omondi na wenzake walikanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya Shilingi 10,000 taslimu za Kenya, sawa na (TSh. 185,000)
Jana Mchekeshaji huyo alitiwa mbaroni pamoja na wenzake kwa kuongoza maandamano hayo ambayo alidai ni kupinga kupanda kwa gharama za maisha ya Mkenya kwenye bidhaa, chakula na mahitaji ya muhimu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live