Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eric Omondi atangaza kupata mtoto akiwa na miaka 41

Omondi Kupata Mtoto Eric Omondi atangaza kupata mtoto akiwa na miaka 41

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchekeshaji Eric Omondi na mpenzi wake wa muda mrefu Lynn wametangaza kutarajia mtoto wao wa kwanza miezi michache baada ya kutangaza kuharibikiwa na mimba yao ya kwanza.

Omondi kupitia ukurasa wake wa Instagram leo ameweka picha nzuri wakiwa na mpenzi wake wake lakini pia ishara ya ujauzito ulikuwa bayana kabisa.

Mchekeshaji huyo alimshukuru Mungu kwa kumwezesha kuishi na hatimaye kukaribia kuona zao lake baada ya miaka 41 ya kutua duniani.

Omondi alijifananisha na hadithi ya Sarah na baba wa Imani Abraham kutoka kwenye Biblia ambao walilazimika kusubiri kwa miongo kadhaa kabla ya kupata mtoto wao wa kimiujiza, Isaka.

“Imenichukua miaka 41 lakini hatimaye Mungu amenibariki na zangu. Tunda la viuno vyangu. Ninahisi kama Sara wa Abrahamu anayetajwa katika Biblia, alingoja maisha yake yote kupata mtoto wake mwenyewe,” Omondi aliandika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live