Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eric Omondi akamatwa tena Kenya

ERIC OMONDIIII Eric Omondi akamatwa tena Kenya

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheshi Eric Omondi alikamatwa Jumatano, Machi 1 alipokuwa akisambaza unga wa mahindi kwa wafuasi wake katika Uwanja wa City Stadium jijini Nairobi.

Mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei alisema wanamhoji na wengine watano waliokamatwa.

Mcheshi uyo maarufu alikuwa amewaalika mashabiki wake kuja kuchukua pakiti ya unga wa mahindi kabla ya maonyesho yake aliyopanga katika Ikulu wiki ijayo.

“Jumatano hii tunakutana katika Uwanja wa City kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa 2 jioni huku tukishiriki pakiti ya unga na kila mtu ambaye ana nia ya kuungana nasi Ikulu. Tunatoa wito kwa watu wenye mapenzi mema kuchangia unga,” Omondi alisema Jumatatu.

Huku akikamatwa, Omondi alijitetea, akisema kuwa Wakenya wengi wanakabiliwa na matatizo ya kiuchumi.

“Wakenya wengi wana njaa. Nilikuwa tu nikisambaza unga huu kwa wahitaji,” alisema.

Alipelekwa katika kituo cha polisi cha Industrial Area kabla ya kufikishwa mahakamani.

Mcheshi huyo maarufu alikamatwa Jumanne wiki iliyopita baada ya kujaribu kuvamia majengo ya Bunge akiwa na kundi la wanaume waliovalia kaptula nyeusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live