Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Enock amfuata Wyre Kenya

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mmoja wa wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band, Enock Bella, anatarajia kuachia kolabo yake ya kwanza na msanii kutoka nchini Kenya, Kevin Waire maarufu kwa jina la ‘Wyre’.

Bella alisema safari ya kuanza kufanya kazi na msanii huyo aliyewahi kutesa na kibao cha’Nakupenda Pia’, ni baada ya yeye kufanya ziara hivi karibuni kwenye vyombo vya habari nchini Kenya kutambulisha wimbo wake wa ‘Mapenzi’.

Kama vile haitoshi alisema ni msanii ambaye alikuwa akitamani kufanya naye kolabo tangu alipokuwa Yamoto lakini kutokana na mkataba uliokuwa ukiwasimamia kama kundi ilishindikana.

“Hata hivyo, nashukuru nilipomtafuta wakati nafika nchini Kenya kumbe naye alikuwa akifuatilia muziki wangu na kunieleza kuwa naye anataka kufanya muziki wa kisasa na hapo ndipo tukakubaliana kufanya kazi kwa kupika kibao ambacho kipo katika mtindo wa dancehall na natarajia kukiachia wiki ijayo,” alisema Bella.



Chanzo: mwananchi.co.tz