Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Endeleza vita na mademu, kwenu tunajaza uwanja bila wewe

Baba Levo Na Harmo Baba Levo.

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya Harmonize kukubali ombi la Diamond kuhudhuria tamasha la Wasafi Festival mwezi huu, chawa wa Diamond, Baba Levo amemkoromea Harmonize na kumtaka kukoma kujihusisha nao.

Baba Levo anahisi kwamba Harmonzie kubadili mawazo yake ghafla na kukubali ombo hilo baada ya kulikataa awali wazi wazi ni kama kujaribu kwenda na upepo.

Baba Levo alimkalifisha vikali Harmonize na kumuambia kuwekeza nguvu hizo anazotaka kuzipeleka kwenye tamasha la Wasafi Festival huko kwao Mtwara, kuzipeleka kwa vita yake na aliyekuwa mpenzi wake Kajala na binti yake.

“Jumamoss Hii MWANZA ITATAJWA List Ya Wasanii A LIST Watakao Kiwasha MTWARA #WASAFIFESTIVAL2023 ..! Wewe Bwana KILANDAGE [Harmonize] USITAKE KWENDA NA UPEPO TAFADHALI..!!” Baba Levo alisema.

Wasafi Festival itaandaliwa mwezi huu ni itafnayika nyumbani kwa kina Harmonize na Baba Levo alimuambia msanii huyo aliyeondoka kwa njia ya kishari mwishoni mwa 2019 Wasafi WCB kwamba watajaza uwanja wa nyumbani kwao wenyewe.

“[Uwanja wa] Nangwanda tutajaza wenyewe, Kirandange [Harmonize] endelea na vita zako za madem,” Baba Levo aisema.

Harmonize na familia ya Kajala wamejikita katika mzozo wa maneno mitandaoni wakijibizana kuhusu penzi lake na mrembo huyo ambalo lilitumbukia shimoni mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live