Mwezi huu wa Aprili, mwaka 2022 rapa Eminem anasheherekea miaka 12 ya kuwa SOBER. Ni miaka 12 bila matumizi ya dawa za kulevya za aina yoyote, bila kunywa pombe au kuvuta bangi.
Mwaka 2008 Eminem aliacha kutumia dawa kama Vicodin, Ambien na Valium baada ya kutumia Methadone kupita kiasi [OverDose] na kuhatarisha maisha yake.
Kwenye interview na VIBE, Eminem alisema kuwa alipewa Methadone na daktari wake, ni dawa inayosaidia watu waliokuwa wakitumia Cocaine na Heroin kwa muda mrefu, ila yeye alitumia dawa hio kupita kiasi bila kujua madhara yake.
Mwaka 2010 alitoa album ya RECOVERY iliyoshinda tuzo ya Grammy ya Album Bora Ya Mwaka, Eminem huwa anatumika kama mfano wa mtu aliyeweza kushinda vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwa watu maarufu.