Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elvis Presley: Ngozi nyeupe, damu nyeusi

Skynews Elvis Elvis Presley

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mwaka 1955, wakati ambao wanamuziki walikuwa wakipiga ngoma mbalimbali nchini Marekani. Wakati huo, meneja wa aliyeitwa Colonal Parker alikuwa akihangaika kutafuta wanamuziki ambao wangemuingizia mkwanja mrefu kibondoni.

Sasa wakati akiwa anatafuta mtu, amekata tamaa ndipo akapelekewa habari na kijana mmoja kwamba kuna msanii mmoja mkali sana, huyu alitakiwa awe naye kwani alionekana pesa nyingi sana mbeleni.

Kwa shauku kubwa akaulizia, ni nani huyo? Akajibiwa ni jamaa mmoja aliyekuwa akiishi huko Memphis. Colonal akashusha pumzi ndefu halafu akaona kama jambo lisilowezekana kuwa na msanii huyo. Kwa nini?

Miaka hiyo nchini Marekani kulikuwa na ubaguzi mkubwa wa rangi na hata ngoma walizokuwa wakitoa basi waliburudishana wao kwa wao. Mzungu anakaaje chini na kumsikiliza mtu mweusi?

Sasa huko Memphis lilikuwa eneo lililokaliwa na wanamuziki wengi weusi, sasa huyu Colonal alipoambiwa huyo mwanamuziki anatoka huko, akajua kabisa alikuwa mtu mweusi.

Nini afanye? Akakataa lakini akaambiwa huyo jamaa ni mweupe. Tena ni hatari sana.

Akashikwa na hamu ya kumuona, halafu amsikilize, alitaka kujua alikuwa na utaalamu gani kwenye kucheza na kinasa sauti. Akaondoka na kwenda kumuona huko alipokuwa akipiga tamasha lakini hakuwa akijulikana sana.

Mwanamuziki huyo ni nani? Anaitwa Elvis Presley, mwanaume aliyewahi kuwa na mtoto ambaye alikuja kuolewa na Michael Jackson, mtoto aliyeitwa Lisa.

Sasa twende kwa pamoja. Colonal akafika mpaka mahali hapo na kuanza kumwangalia huyo jamaa. Alikuwa back stage na familia yake, kama kawaida ya wenzetu, hata kama muziki wao haukuwa wa kumtukuza Mungu, kwanza walishikana mikono na kuanza kusali. Kila kitu walikikabidhi mikononi mwa Mungu aliye hai.

Ni bwana mdogo tu, hakuonekana kuwa na uhatari wa kupiga muziki, alionekana wa kawaida kiasi cha Colonal kuhisi kama ameingizwa choo cha kike ila baada ya kutumbuiza jukwaani, sasa akaona hii pesa. Huyu hatakiwi kuachwa.

Akataka kuonana naye na kuzungumza, ilikuwa ni lazima amwambie ukweli ili tu ajue kwamba alikuwa akienda kunukia kwenye mafanikio makubwa kama tu angepiga kazi naye.

Hold on! Huyu dogo ilikuwaje huko nyuma? Elvis alizaliwa kwenye familia ya kimasikini tu, ambayo haikuwa ikijua mbele waka nyuma ya maisha yao. Waliishi hivyo na dogo alipania sana kufanya muziki ili kuitoa familia yao kutoka huko kwenye bwawa la umasikini.

Sasa walizungukwa na watu weusi, hata washikaji zake walikuwa ni weusi tu. Kwa kuwa alipenda sana kuimba, alipenda sana kwenda kanisani, alifurahi kuwasikia watu wakiimba.

Kwenye wanamuziki waliokuwa wakifanya muziki, Elvis alitokea kumkubali sana B. B King. Huyu alikuwa mwanamuziki mweusi aliyekuwa akipiga ngoma nyingi kali.

Hakuwa akijulikana kwa sababu muziki wake alikuwa akiwafanyia watu weusi. Hata kipindi ambacho Elvis alitoka, alipiga sana ngoma za huyu jamaa. Yaani kwa kufupi alikuwa Role Model wake.

Sasa akakutana na Colonal na kuanza kuzungumza. Jamaa alimuahidi mambo mengi, kuwa tajiri, kuwasaidia wazazi wake na hata kuwanunulia gari aina ya Cadillac ya rangi ya pink.

Kwa miaka hiyo ulipokuwa unalitaja Cadillac lilikuwa gari la kishua, huwezi kuendesha kama shule ya sekondari umesoma syllabus ya akina Mabala The Farmer, ilikuwa gari ya kifahari, ili uipate ni lazima uwe mwanasiasa na upige pesa za walala hoi.

Sasa hiyo ndiyo gari ambayo dogo aliambiwa akiungana na Colonal, mbona kitu chepesi sana. Akakubali.

Ni kweli akapata alichokitaka, akatoa ngoma nyingi kali lakini serikali ni kama haikumkubali. Unajua kwa nini? Nitakujibu.

Hawakumkubali kwa sababu alikuwa na urafiki mwingi na watu weusi, yaani alikuwa akiwapenda sana na hii ni kwa sababu tu alikulia kwenye mitikasi ya watu hao.

Akaandaliwa mpaka tamasha ambalo lilikuwa na bango lenye bendera za kuushinikiza ubaguzi wa rangi, na ilikuwa ni lazima afanye kwa sababu serikali ilipanga hivyo.

Miaka ikasogea, akaja kupata mke aliyeitwa Priscilla, huyu nitakuja na stori yake siku nyingine tuone ilikuwaje mpaka kukutana na huyu mwamba.

Kwa hiyo kwa kumwangalia Elvis alikuwa Mzungu lakini damu yake ilikuwa ni ya watu weusi. Alifanikiwa, aliwapenda na kuwakumbatia ila jamaa baadaye alikufa kufariki dunia.

Baadaye ikambidi aondoke zake na kwenda Ulaya. Alikwishaona Marekani ni magumashi na lingekuwa jambo gumu sana kupiga hatua kwa sababu walimuwekea zengwe kubwa.

Alikaa huko kipindi kirefu na aliporudi, akaamua kujiingiza kwenye masuala ya filamu. Huyu alikuwa mwamba, hata huko alionekana kuwa mwiba wa kuotea mbali. Ila kipaji ni kipaji tu, akaamua kurudi kwenye muziki na kuendelea na mitikasi yake.

Mpaka leo hii jina la Elvis ni kubwa sana, ana ngoma kali sana ambazo nyingine ilifanywa tena na UB40 iitwayo Can’t Help Falling In Love.

Unajua nini kilimuondoa? Kila mmoja alikuwa anasema lake. Baada ya kupata umaarufu, pesa na kila kitu alichokihitaji, jamaa akaanza kutumia madawa ya kulevya. Ni kama mwanamuziki wetu mzee wa migodi.

Sasa hilo ndilo lilimuumiza, alipata kila kitu, madawa kwa wingi na akawa mtu wa mademu kishenzi. Lilikuwa jambo la kawaida kuwala mate wanawake jukwaani mbele ya mkewe, jamaa alichanganyikiwa sana.

Baadaye mwaka 1977 mshikaji akafariki dunia. Hapa kuna ripoti mbili. Ripoti ya kwanza ya kitabibu inasema mchizi alikufa kutokana na moyo wake kushindwa kufanya kazi lakini wengine sasa ambao si madaktari walisema kwamba madawa ya kulevya ambayo alikuwa akitumia mara kwa mara ndiyo yaliyomuua.

Jamaa alifariki na kuacha mtoto mmoja, Lisa ambaye naye alifariki mwaka 2022 na kuacha watoto wawili, Riley Keough mwenye miaka 34 ambaye ni muigizaji na ameonekana kwenye muvi kama Mad Max, Devil All The Time, Logan Lucky na nyinginezo. Pia alikuwepo Benjamin Keough aliyefariki mwaka 2020.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live