Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Elon Musk afunguliwa kesi nzito

Jaji Azuia Mpango Wa Malipo Wa $56bn Kwa Elon Musk 'usioeleweka' Elon Musk afunguliwa kesi nzito

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watendaji Wakuu wa Mtandao wa X (zamani Twitter) ambao walifukuzwa kazi baada ya Elon Musk kuununua Mtandao huo, wamefungua Kesi ya madai wakimtaka Bosi huyo mpya kuwalipa Dola Milioni 128 (zaidi ya Tsh. Bil. 326) kwa kuwaondoa kazini kikatili

Kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya San Francisco walalamikaji wakiwa ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Twitter, Parang Agrawal pamoja na Watendaji wengine watatu wanaodai kuwa Elon alivunja haki za Wafanyakazi waliofukuzwa baada ya kuinunua kampuni hiyo

Taarifa zaidi zinadai hadi kufikia Mwaka 2021, Agrawal alikuwa na madai ya fidia yenye thamani ya zaidi ya takriban Tsh. Bilioni 76.5 kutoka katika kampuni hiyo.

Ikumbukwe, wakati Elon akiwaondoa kazini alisema Watendaji hao walikuwa na uzembe mkubwa na utovu wa nidhamu wa makusudi na hivyo halazimiki kuwalipa fidia yoyote

Chanzo: www.tanzaniaweb.live