Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Elon Musk: Bosi wa Tesla ameuza 10% ya hisa za Tesla kwa Tsh. trilioni 11.5

Elon Musk Tesla Shares Twitter 1200x900 Elon Musk: Bosi wa Tesla ameuza 10% ya hisa za Tesla kwa Tsh. trilioni 11.5

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji mkuu wa Tesla na tajiri namba moja duniani, Elon Musk ameuza hisa zake kwenye kampuni hiyo inayounda magari magari ya umeme.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya kuwauliza wafuasi wake milioni 63 wa Twitter kama anapaswa kuuza 10% ya hisa zake katika Tesla.

Hisa za kampuni hiyo zilishuka kwa karibu 16% katika siku mbili baada ya kura ya maoni iliyounga mkono yeye kuuza hisa, kabla ya kupata faida siku ya Jumatano November 10.

Kampuni ya Tesla ni mtengenezaji wa magari ya umeme yenye thamani zaidi duniani, na tathmini ya soko la hisa inaonesha kumiliki zaidi ya dola trilioni 1.

Musk ameuza karibu hisa milioni 3.6 za Tesla, zenye thamani ya karibu $4bn.

Pia aliuza hisa nyingine 934,000 kwa takriban Tsh. trilioni 3 baada ya kutumia chaguzi za kupata karibu hisa milioni 2.2, kulingana na faili zilizowasilishwa na mdhibiti wa soko la hisa la Marekani

Chanzo: www.tanzaniaweb.live