Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elba kufungua studio ya filamu Bongo

Elba Kufungua Studio Ya Filamu Bongo Elba kufungua studio ya filamu Bongo

Mon, 30 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus amesema mazungumzo ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia na Muigizaji Maarufu wa Filamu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD waliyoyafanya Wiki iliyopita Davos nchini Uswizi yamezaa matunda na tayari Elba ameonesha nia ya kufungua studio kubwa ya Filamu Tanzania.

Akiongea Ikulu Dar es salaam leo kuhusu ziara ya Rais Samia nchini Uswizi na Senegal, Zuhura amesema;

“Rais Samia alikutana na Idris Elba na Mkewe Sabrina ambao wao katika Uwekezaji wanataka kuja kuwekeza kuanzisha studio kwa ajili ya Filamu, kwa hiyo mazungumzo ndio kwanza yanaanza lakini yakifanikiwa ina maana hiyo studio itaweza kusaidia sio tu Tanzania lakini Afrika Mashariki na kati.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live