Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ed Sheeran ashinda kesi yake dhidi ya Marvin Gaye

17)Marvin Gaye Eddy S.jpeg Ed Sheeran ashinda kesi yake dhidi ya Marvin Gaye

Fri, 5 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Manhattan, New York nchini Marekani imetoa uamuzi wa kesi iliyokuwa ikimkabili Staa wa muziki wa nchini Uingereza Ed Sheeran na kusema wimbo wake maarufu wenye zaidi ya views bilioni 3.5 kwenye YouTube “Thinking Out Loud” haukukiuka hakimiliki za wimbo wa Mwimbaji wa Marekani Marvin Gaye uitwao “Let’s Get It On.”

Baraza la Mahakama limesema Ed Sheeran alitunga na kutengeneza wimbo wake kwa kujitegemea na hakuna kipengele chochote kwenye utunzi wa nyimbo hiyo kilichotoka kwenye wimbo wa Marvin Gaye.

Kesi hii ilishika kwenye headlines duniani baada ya mashtaka hayo dhidi ya Ed Sheeran kufunguliwa mwaka 2017 ila hatimaye uamuzi ulitolewa mapema hii leo kuhusu sakata hili ambalo Ed Sheeran aliwahi kuweka ahadi ya kuacha kufanya muziki endapo angekutwa na hatia ya kuiba wimbo wa Marvin Gaye.

Ndugu wa mtunzi mwenza wa nyimbo ya Marvin Gaye walimfungulia kesi Sheeran wakidai kwamba mdundo wa sauti wa nyimbo hizo mbili ulikuwa unafanana wakisema Ed Sheeran alikiuka hakimiliki ya wimbo yao ambapo kama Ed Sheeran angekutwa na hatia angetakiwa kuwalipa Walalamikaji dola milioni 100 kama fidia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live