Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ed Sheeran ajenga kaburi atakalozikwa

Ed Grave Ed Sheeran ajenga kaburi atakalozikwa

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Ed Sheeran amefichua kuwa tayari amejenga kaburi lake nyumbani kwake Uingereza huku akitoa sababu za kufanya hivyo.

Mwimbaji huyo ameweka wazi kwenye mahojiano na GQ, huku akisema kuwa kaburi lake ni la kawaida sana ambalo limechimbwa shimo huku juu limewekewa jiwe, na akakazia kuwa siku akifariki atumbukizwa humo.

Hata hivyo Ed Sheeran amedai kuwa kufanya hivyo watu wanafikiri ni jambo la ajabu na la kuhuzunisha lakini amekuwa akishuhudia marafiki zake wakifarki na kuwaacha watu wasijue nini cha kufanya.

Si kaburi tu lakini pia mwanamuziki huyo amejenga kanisa dogo nyumbani kwake hapo ambalo limekamilika likiwa pamoja na kaburi hilo huku akidai kuwa lengo kuu la kufanya hivyo pia itasaidia watoto wake kumkumbuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live