Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

EX msumbufu atupwa jela miaka mitano

Jela 1.jpeg EX msumbufu atupwa jela miaka mitano

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja kutokea Jimbo la Maryland nchini Marekani huenda akafungwa hadi miaka mitano Jela iwapo atakutwa na hatia ni baada ya kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa mitandao dhidi ya mpenzi wake wa zamani (EX) ikiwa ni pamoja na kumsumbua EX wake kwa kumpigia simu kwa zaidi ya mara 800 ndani ya siku mbili.

Derik Wayne Bowers (44) alishtakiwa mwanzoni mwa wiki hii kwa kosa la kumsumbua EX wake kupitia mitandao (Cyberstalking) na kumnyanyasa EX wake kupitia ujumbe mfupi wa sms, kumsumbua kwa kumpigia simu na unyanyasaji kupitia mtandao wa Facebook.

Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani katika Wilaya ya Kaskazini mwa Virginia Magharibi imesema December 2022, Bowers alimpigia simu EX wake ambaye anaishi katika Kaunti ya Morgan, Marekani mara 815 kwa muda wa siku mbili, huku ikisemekana kuwa alimtumia maelfu ya ujumbe kwa muda wa miezi kadhaa na alitumia post kupitia mitandao ya kijamii kumuaibisha na kumfuatilia maisha yake.

Mwanamke huyo anadai hajawahi kukutana na usumbufu wa aina hiyo tangu amezaliwa na iwapo Derik Wayne Bowers ambaye kwa sasa yupo Mahabusu, atapatikana na hatia hiyo atafungwa hadi miaka mitano Jela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live