Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EP ya Diamond FOA yaobekana kwenye basi Uingereza

Diamond Uk Foa FOA EP ya Diamond yaobekana kwenye basi Uingereza

Fri, 15 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa @diamondplatnumz anaendelea kutunisha misuli Kimataifa. Mara hii ni kuhusiana na tangazo la EP yake "First Of All" ama #FOA kuwa kwenye usafiri wa umma huko Uingereza.

Hilo limewekwa wazi na meneja wa mkali huyo Sallam SK ambaye kwasasa yupo na Diamond huko London, Uingereza kwaajili ya shughuli zao za kimuziki.

@sallam_sk ame-share kupitia insta story yake Basi hilo lenye tangazo la EP ya Diamond likiwa kwenye mitaa ya huko London, Uingereza.

Diamond ambaye aliwahi kusema hapendezwi kushindanishwa na wasanii nchini kutokana na kuwazidi katika maeneo makuu matatu; ambayo ni mauzo, shoo za kimataifa na maendeleo (mali) yatokanayo na muziki, hii ni hatua nyingine anayoionyesha kuwa anaimba na kutafuta wateja wakumsikiliza popote duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live