Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EFM yachanja mbuga, watua Dodoma, Morogoro

8553 2 TZW

Sun, 3 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Kituo cha redio cha EFM ambacho kilianzishwa miaka 4 iliyopita ndani ya Jiji la Dar es salaam Dar es salaam (93.7), kinazidi kuchanja mbuga baada ya wiki hii kuanza kurusha matangazo katika mkoa wa Dodoma kupitia masafa ya 92.5 pamoja na Morogoro kupitia 95.5.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Mahusiano wa kituo hicho, Jesca Mwanyika amesema wanayofuraha ya kuwalika Wanadodoma kuanza kusikiliza EFM kwani licha ya kutoa burudani na kuelimisha, wasikilizaji huwezeshwa kiuchumi kupitia matamasha mbalimbali ambayo huandaliwa kituo hicho.

“Efm redio kwa kutambua uhitaji wa jamii wa kupata matangazo yao, burudani na matamasha mbalimbali ambayo yamejikita katika uwezeshaji wanatarajia kuongeza masafa yake na kusikika Tanzania nzima, baada ya Dodoma na Morogoro hivi karibuni tunatarajia kutambulisha masafa mengine mapya kwa mkoa wa Kigoma na Tabora,” alisema Jesca.

Alisema kuwasha mitambo Dodoma na Morogoro ni mwendelezo wa kutaka kuwafikia Watanzania wengi zaidi ili waendelee kuisikiliza na kushiriki katika matamasha mbalimbali yanayoandaliwa na redio hiyo kwani ni redio iliojikita katika kuinua uchumi wa mwananchi.

Matambasha ambayo yanaadaliwa ya kituo hicho ni Muziki Mnene, Shika Ndinga pamoja na Sakasaka ambalo msimu wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wiki mbili zilizopita wakati wa fainali ya Tamasha la Shika Ndinga, mgeni rasmi wa shindani hilo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe alisema kituo hicho anakipongeza kwa kazi wanazozifanya pamoja na hatua ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kupitia matamasha yao.

Loading...
Chanzo: bongo5.com