Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duma, Gabo kimeumana tena!

GAMBO DUMA Duma, Gabo kimeumana tena!

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Filamu Bongo, Daud Michael maarufu 'Duma' ameweka wazi kuwa popote atakapokutana na msanii mwenzie Salim Ahmed Issa ‘Gabo’, asimsalimie wala kumpa mkono, kwa sababu wawili hao wanaugomvi wa muda mrefu.

Duma amesema hayo akidai kuwa ugomvi wao haujawahi kuisha lakini ameshangaa hivi karibuni kwenye harusi ya msanii mwenzao Barnaba pale Mlimani City, Gabo alimfuata na kumpa mkono jambo ambalo anadai kuwa ni salam ya kinafiki.

“Ni jambo zito, mimi na Gabo hatuko sawa muda mrefu na Watanzania wanajua. Kutokuwa sawa na mtu sio kosa, mimi na Gabo tumekutana sehemu nyingi sana tofauti, yeye anapita huku mimi kule wala hakuna makele na maisha yanakwenda.

“Lakini ikumbukwe Gabo alishawahi kuja kupasua gari yangu vioo pale Bongo Movie, na nilimsamehe maisha yakaendelea.

“Kilichonishangaza nakumbuka dada yangu Monalisa alikuwa ametupanga kwenye meza ya wasanii na Linah, Mwijaku, Simple The Boy, tulikuwa wengi, nikashangaa gabo akaja akanipa mkono tusalimiane.

“Nilikuwa nimeinama nachati ninaiua macho namuona Gabo, nikajiuliza ni nini? Nikasema acha nimsalimie nikampa ngumi, akaondoka zake. Nikawapigia management yangu wakaniambia hapo sio salama ondoka, nikaondoka hata sikula, nilijiuliza sana.

“Nataka hili jambo Watzania walielewe, simchukii gabo lakini sitaki mazoea naye, ile ilikuwa unafiki kwa vile kuna watu ionekana hawa huwa wanagombana, Gabo amekuja kumsalimia Duma lakini amekataa, Duma ndiyo aonekane mkorofi, Gabo mstaarabu,” amesema Duma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live