Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dully ataka Serikali iutangaze zaidi Mlima Kilimanjaro

DULLY NA MLIMA KILIMANJARO Dully na Mlima Kilimanjaro.

Sun, 26 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Legendari wa Bongo Fleva, Abdul Sykes 'Dully' ametoa mawazo yake ya kuitaka Serikali iongeze kasi katika kuutangaza Mlima Kilimanjaro kwani bado watu wengi nje ya Tanzania wanaamini upo Kenya badala ya Tanzania.

Dully ametoa maoni yake hayo kupita ukurasa wake wa Instagram ambapo pomoja na mambo mengine amesema hata Kiswahili kinapaswa kutangazwa zaidi kijulikane asili yake ni Tanzania.

"Kuna kitu bado Serikali inapaswa kufanya. Wapo watu wanaamini Mlima Kilimanjaro upo Kenya kitu ambacho sio sahihi," amesema Dully.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live