Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dully amshukuru Diamond kumpigia simu

Dully Na Mondi Dully amshukuru Diamond kumpigia simu

Sat, 10 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Legendari Dully Sykes, amefunguka kuwa anamshukuru Mungu Diamond amempigia simu na kumwabia wafanye naye ngoma.

Akizungumza na Wasafi TV, Dully alisema, kabla hajafika kwenye mahojiano aliyofika kuyafanya, Diamond alimpigia simu na kumuambia wakifika amuone ofisini kwake.

“Namshukuru Mungu Diamond alinipigia simu akaniambia nikifika tu hapa nimuone na kwa kweli nimwaambie, tunakwenda kufanya ngoma nyingine na ameniambia itakuwa ni Dully featuring Diamond,” alisema Dully.

Wimbo huo utakuwa wa pili Dully kufanya na Diamond, awali aliwahi kufanya naye wimbo uliokwenda kwa jina la Utamu akiwa amemshirikisha pia Ommy Dimpoz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live