Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dully Sykes alivyomtoa Diamond kimziki

DULLY DIAMOND Dully Sykes alivyomtoa Diamond kimziki

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alianzisha Dhahabu Records na baadaye Studio 1.12. Studio zake zimetoa ngoma maarufu Bongo kama Mdananda ya Shetta, Ameen ya Mwana FA, Dar es Salaam Stand Up ya Chidi Benz na nyinginezo.

Dully Sykes ametoa albamu kama Historia ya Kweli (2003), Handsome (2004), Hunifahamu (2005) na anatajwa kama miongoni mwa waanzilishi wa Bongofleva. Twende kazi.

1. Hadi Dully Sykes anatoka kimuziki alikuwa anafanya kazi ya kuuza kanda (tape) dukani kwa DJ Lover (Guru) na ndiye aliyekuwa meneja wake wa kwanza kimuziki.

2. Baada ya Abby Skills kugundua kipaji cha Mr. Blue aliamua kumkutanisha na Dully Sykes ambaye ndiye alimpeleka studio kwa DJ G Lover, G Records na kuanza kurekodi hadi akatoka kimuziki na ngoma yake, Mapozi.

3. Wimbo wa Dully Sykes ‘Julieta’ ndio wimbo wa kwanza wa Bongofleva wa kuimba, kwani awali muziki uliokuwa ukifanyika ni wa rap zaidi ingawa Dully naye mwanzo alifanya rap kama ilivyokuwa kwa Jux, Diamond Platnumz na Lady Jaydee.

4. Dully Sykes ndiye alimshawishi Inspector Haroun kumshirikisha Nandy katika wimbo wake ‘Sharubu za Babu’ wakati huo Nandy alikuwa anafanya kazi studio kwa Dully na huo ukawa mwanzo wa mafanikio yake.

Kwa ujumla Dully ana mchango kutoka kimuziki kwa mastaa Bongo kama Alikiba, Young Dee, Queen Darleen, Marioo, Shetta, Mr. Blue na Diamond

5. Baada ya Mr. Blue kugundua kipaji cha Young Dee, naye akampeleka kwa Dully Sykes ambaye alimpa jina hilo (Young Dee) kisha kumpeleka studio kwa Lamah, Fishcrab ndipo akatoka kimuziki na kila mtu kumfahamu.

6. Dully Sykes ndiye chimbuko la jina ‘Sharobaro’ ambalo kwa mara ya kwanza alimpa Hakeem, baadaye jina hilo lilikuja kutumiwa na Bob Junior kwenye muziki na studio yake, Sharobaro Records.

7. Ukishangaa kwanini hadi leo Snoop Dogg hajawahi kushinda Grammy licha kuchaguliwa kuwania mara 20, pia kumbuka hadi sasa Dully Sykes hajawahi kushinda tuzo Bongo - zile za Tanzania Music Awards (TMA) licha kuchaguliwa kuwania zaidi ya mara tano tangu mwaka 2004. Hiyo ni sawa na Mr. Blue, Juma Nature na TID.

8. Kuna nyimbo mbili ambazo Dully Sykes ameshirikishwa ziliwahi kushinda tuzo Bongo nazo ni ‘Action’ ya C Pwaa iliyoshinda tuzo mbili za KTMA 2011 na pia kuna ‘Maneno Maneno’ ya Queen Darleen’ iliyoshinda kama Wimbo Bora wa Ragga & Dancehall 2012.

9. Queen Darleen alianza kuwika kimuziki baada ya kushirikishwa na Dully Sykes katika wimbo ‘Historia ya Kweli’ ila tayari sauti yake ilikuwa imesikika kwenye wimbo wa Inspector Haroun, ‘Mtoto wa Geti Kali’ ambao hakutajwa kama ameshirikishwa.

10. Baada ya Diamond Platnumz kurekodi wimbo wake ‘Kamwambie’ mtu wa kwanza kumpelekea na kuusikiliza alikuwa ni Dully Sykes ambaye alimshauri akafanye video kwa Director Adam Juma. Alipouachia wimbo huo ukafanya vizuri hadi Chibu kushinda tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kama Msanii Bora Chipukizi 2010.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live