Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dully Sykes: Wasanii wengine wananiita mjinga

DULLY DIAMOND Dully Sykes: Wasanii wengine wananiita mjinga

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes ameamua kuvunja ukimya kufuatia baadhi ya wasanii wenzake wa zamani kumuona yeye kama mjinga anavyokuwa anafanya kazi na wasanii wa kizazi kipya.

Dully ambaye kwa nyakati tofauti ameonekana akifanya kazi na wasanii kama Kusah, Young Lunya na wengine, ameeleza hayo kupitia insta story yake, akiwaambia wenzake kuwa, kufanya kazi na wasanii hao sio kwamba ni kujishusha au ndio uwezo wao umeisha.

"Watambue kwamba kuna muda wanapaswa wakubali kila kitu kina wakati wake, hivyo waishi kutokana na kizazi kinavyobadilika," ameleza Dully Sykes.

Pia ameendelea kueleza kwamba hawa wasanii wa leo walijifunza kutoka kwao, na wao ni wakubwa zao, hivyo waishi nao tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live