Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dully Sykes: Diamond amefuata njia zangu

DULLY DIAMOND Dully Sykes: Diamond amefuata njia zangu

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Dully Sykes amedai kuwa yeye ni muoga wakufeli katika maisha yake na ni jambo ambalo limemsaidia sana hadi kufika hapo alipo, jambo ambalo hata Diamond Platnumz amelisema kwake.

Dully ameeleza hayo akitolea mfano wa wasanii wenzake wakongwe ambao amekuwa nao kwenye game muda mrefu na walipata pesa nyingi kuliko yeye lakini kwa sasa hawana nafasi ambayo anayo yeye kwa sasa kwenye maisha ya muziki na ya kawaida.

“Kuna wasanii walipata hela kunishinda mimi na nilitamani kuwa kama wao kipindi hicho, kupata zile hela ujue mimi sijawahi kupata mahela kibao kwa wakati mmoja lakini zile pesa ndogo ambazo mimi nilizipata niliweza kwenda nayo na majukumu yangu.

“Mimi ni muoga sana wakufeli nafikiri hata #Diamond alifuata hizi njia zangu pia na yeye ni muoga sana wakufeli. Kuna watu walikua wanatuambia sana tungeweza kuwasikiliza nafkiri sasa hivi tungekua mbali.

“Mimi sasa hivi nawaombea vizuri kwa mwenyezi mungu warudi tena wafanye ngoma zirudi tena warudi kwenye nafasi tena ili wajipange tena pale ambapo wanajua walikosea ili wasikosee tena. Hivyo nawaombea sana kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu sifurahii kuona wenzangu wamepotea.

“Sasa hivi wapo katika maisha flani na wanahitaji msaada, mimi natamani Mungu afanye maajabu yake warudi kwenye nafasi zao wafanye maisha yani nitafurahia sana," amesema Dully.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live