Baada ya kuitumikia EATV LIMITED kwa miaka 15, MC na Mtangazaji nguli Abdallah Ambua maarufu kama Dullah Planet siku ya jana ametangaza rasmi kuikacha kampuni hiyo maarufu ya utangazaji.
Kwenye mazungumzo yake Dullah amesema; "Niombe radhi kwa yeyote nitakayekuwa nimemkwaza katika miaka yangu 15 ya utumishi pale Eatv Africa TV/Eatv Africa Radio kwasababu binadamu tunatofautiana kufikiria, unaweza ukafanya kitu kwa nia njema mwingine ikamkera na ikapelekea kukuchukia kabisa.
"Najua nimefanya kazi nzuri najipongeza mwenyewe. Kwa sasa nitaenda break kidogo najua maswali yatukuwa mengi kuuliza naenda wapi au radio gani? Ikifika time ya come back kila mmoja atajua na ataelewa Dullah anafanya nini," amesema Dullah Planet.