Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dulla Makabila atoa jiwe lingine zaidi ya Pita Huku

Dulla Makabila Atoa Jiwe Lingine Zaidi Ya Pita Huku Dulla Makabila atoa jiwe lingine zaidi ya Pita Huku

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa unaona ataishiwa kwa ngoma za ujumbe baada ya Pita Huku jua ulikuwa unakosea, Dulla Makabila ameachia ngoma nyingine kali inayokwenda kwa jina la Nije ama Nisije.

Wimbo una masaa kadhaa tu huko mjini YouTube na tayari umekamata nafasi ya tano, umeifunika hata Mtaalam ya Lulu Diva aliyomshirikisha Nandy.

Huu ni mwendelezo mzuri wa nyimbo za Singeli zenye ujumbe kutoka kwenye ubongo wa Dulla Makabila, kwenye wimbo huu amemjengea taswira mama ambaye hajali malezi mazuri na kujikuta akitembea na wanaume tofauti, akimtesa mwanaye angali akiwa tumboni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live