Msanii maarufu wa Singeli, Dulla Makabila amethibitisha kuwa ameachana na mkewe Zaylissa baada ya kumuandikia talaka tatu kutokana na ugomvi ulioibuka baina ya wanandoa hao.
Inadaiwa kuwa wawili hao ambao walifunga ndoa mnamo Mei 2021, wamegombana huku Dulla akidaiwa kumshushia kipigo mrembo huyo ambaye ni muigizaji wakati chanzo kikidaiwa kuwa ni Zailissa kukutwa na meseji za ex wake.
Akithibitisha hilo, Makabilla amesema; “Ni kweli hatuko pamoja, siwezi kuanza kuzungumzia chanzo kwenye vyombo vya habari, mimi ninamheshimu sana mtu ambaye nimeshakuwa naye kwenye mashusiano ya ndoa kwa hiyo siwezi kuelezea ni au vile.
“Kifupi ni mwanamke mzuri lakini kuna vitu tu ambavyo tumeshindwana na kuna vitu ambavyo kwangu nimeona kama tumeenda against kidogo. Lakini ni mwanamke mzuri ambaye anafaa lakini siwezi kzungumzia mapungufu yake.
“Tumeshindwana kweli lakini siwezi kumzungumzia vibaa Zay, haina maana kwamba atashindwana na mwingine, ni kweli nimempa talaka tatu. Upendo upo bado lakini kuna vitu nimeshindwa ndio maana tukafikia huko.
“Ninamtakia tu kila la kheri kwa sababu hajanifanyia baya kubwa. Mimi ndio nilioa na nimempa talaka tatu na sihitaji kuzungumza sababu labda yeye aseme, wala sio ishu ya kumkuta na meseji za mwanaume kwenye simu ni mambo mengine tu,” amesema Dulla Makabila.