Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dulla Makabila amchana Mwijaku 'Baba Levo sio mhuni mwenzako'

Dulla Makabila Amchana Mwijaku 'Baba Levo Sio Mhuni Mwenzako' Dulla Makabila amchana Mwijaku 'Baba Levo sio mhuni mwenzako'

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Dulla Makabila amemjia juu mtangazaji Mwijaku kutokana na kauli yake ya kukosoa wimbo wake mpya unaofahamika kama Pita Huku.

Baada ya DC wa Insta Mwijaku kuuponda wimbo huo na kusema kuna baadhi ya vitu kaviimba haviendani na maadili ya Nchi, sasa Hit Maker wa Ngoma hiyo Dulla Makabila ameamua kumvulia uvivu Mwijaku na Kukaa upande wa Baba Levo ambaye alionesha kupendezwa na wimbo huo.

"Mwijaku, Baba Levo akiwa anakuelewesha vitu kuhusu sanaa ya uimbaji uwe unasikiliza sababu wewe sio muimbaji ila yeye muimbaji na kingine Mwijaku usipende kubishana na Baba Levo kwa sababu yeye sio muhuni mwenzako ila tasnia tu imewakutanisha," ameandika Dulla Makabila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live