Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dulla Makabila: Kumuomba Diamond msamaha najua Majjizo atakasirika

Dulla Majizzo Dulla Makabila: Kumuomba Diamond msamaha najua Majjizo atakasirika

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Singeli, Dulla Makabila amesema kitendo chake cha kumuomba msamaha supastaa wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya Wasafi, Diamond Platnumz huenda kimemkasirisha CEO wa E Radio na ETV, Fracis Antony Ciza Majey 'Majizzo'.

Akizungumza na wanahabari katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba msanii huyo amesema namna alivyotunga wimbo kwa ajili ya kumuomba Diamond radhi ili amrejeshe tena katika ushikaji wake na WCB na Wasafi Media.

“Najua nilimkosea Diamond na kabla ya kutoa wimbo niliomba ushauri ili isijekuonekana kama nakifanya naomba msamaha ili nitoe wimbo. Najua Majizzo atakasirika ila sina tatizo naye,” aliongeza Dulla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live