WALIOSEMA sikio la kufa wala hawakukosea, kwani ikiwa imepita muda mchache tangu achomolewe kwenye adhabu, mwimbaji maarufu nchini, Godfrey Tumaini 'Dudubaya', amejikuta akiingia tena matata na tayari Baraza la sanaa Taifa (Basata) limemuandikia barua. Basata limemuandikia barua staa huyo wa 'Mwanangu Huna Nidhamu' kumuita ili kwenda kujieleza kwao kutokana na kutumia lugha isiyo ya staha kwenye mitandao ya kijamii. Dudubaya anatakiwa kuripoti keshokutwa Jumanne kwenye ofisi za makao makuu ya Baraza hilo Mwimbaji huyo mtata, ameiposti barua hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram na kukubali wito huo siku ya Jumanne. Hii si mara ya kwanza Dudubaya kuitwa na Baraza hilo kutoka na matumizi ya lugha za matusi mtandaoni. April 10,2020 Dudubaya kwenye akaunti yake ya Instagram aliposti video ikimuonyesha anatoa lugha ya matusi kwa baadhi ya Media kwa madai hawakuripoti habari iliyotolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shoza inayohusu mshindi wa BSS 2019 Meshark Fukuta kutolipwa pesa zake na kampuni ya Benchmark 360 ltd iliyoendesha shindano hilo.