Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dudubaya akimaliza polisi, kuhojiwa Basata

44367 Dudupic Dudubaya akimaliza polisi, kuhojiwa Basata

Sun, 3 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Licha ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi, msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kwa jina la Dudu Baya, pia anasubiri kuitwa mbele ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Hayo yamesemwa leo na Machi 1, 2019  na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, ikiwa ni siku moja tangu isitishe usajili wa msanii huyo.

Akizungumza na Mwananchi, Mngereza amesesema kusitisha usajili wa msanii huyo ni hatua ya kwanza lakini pia watamuita kumhoji baada ya kumalizana na Jeshi la Polisi ambalo lilimkamata jana na kumuachia kwa dhamana katika kituo cha Oysterbay.

"Hata kazini kwako ukiwa umemwajiri mtu na unaona anafanya mambo ambayo siyo kuna hatua unapaswa kuzichukua ikiwemo kumsimamisha kwa ajili ya uchunguzi.

"Hivyo ndivyo pia tumefanya Basata kusitisha usajili wa Dudubaya ambaye sasa hataruhusiwa kujishughulisha na kazi zozote za sanaa, lakini pia tunasubiri amalizane na polisi na sisi tutamuita kumhoji ili kujua ana tatizo gani.

"Kwa anachokifanya msanii huyu lazima kama binadamu wa kawaida ujiulize ana nini na kwa kuwa kesi yake ipo polisi kwa sasa tunasubiri wamalizane naye," amesema Katibu huyo.

Alipoulizwa kwa nini wamechukua hatua ya kumsitishia usajili kabla hawajabaini kama ana makosa au la huko polisi, Mngereza amesema wanachofanya ni kutekeleza maagizo ya Waziri mwenye dhamana ya kusimamia sanaa.

Amebainisha kwamba katika maagizo ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, siku mbili zilizopita aliliagiza Jeshi la Polisi na Basata kumchukulia hatua, hivyo kama Basata na wao wametekeleza maagizo hayo.

Wito wake kwa jamii, endapo wanaona wamekosewa na wasanii wasisubiri Basata lichukue hatua na badala yake waende kutoa malalamiko yao kwenye vyombo husika kwani nchi inaongozwa na sheria.

Dudu Baya aachiwa kwa dhamana



Chanzo: mwananchi.co.tz