Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dudubaya afikishwa Mahakamani

Pic Dudubaya Data Dudubaya afikishwa Mahakamani

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Mwanamuzi wa bongofreva Godfrey Tumaini maarufu Kama (Dudubaya) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la lugha chafu mtandaoni.

Dudubaya (41) Mkazi wa Mbezi alipandishwa kizimbani Mahakamani hapo na kusomewa hati ya Mashtaka na Wakili wa Serikali Hilda Katto mbele ya Hakimu Mkazi Ester Mwakalinga.

Wakili amedai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 11, mwaka 2020 akiwa nchini Tanzania .

Aliendelea kudai, mshtakiwa Dudubaya aliandika lugha ya matusi kwa Joseph Kusaga katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuisambaza.

Mbali na hapo mshtakiwa alikana kutenda, kwa upande wa Jamhuri Wakili amedai upelelezi umekamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe kwa ajili ya kusikilizwa.

Kutokana na shauri kudhaminika , Hakimu Mwakalinga alimpangia mshitakiwa masharti ya dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaokidhi vigezo vya Mahakama sambamba na kutia saini bondi ya sh. milioni 2.

Dudubaya yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti na kesi itasikilizwa Januari 28, 2021.

ASKARI POLISI AJINYONGA KWENYE NYUMBA INAYOJENGWA “ALIKUWA MTU WA WATU”

Chanzo: millardayo.com