Msanii nguli wa Bongo Fleva, Dudu Baya atoa somo kwa wasanii wachanga, adai alizungushwa wiki 6 na Master J kurekodi wimbo ‘Mwanangu Huna Nidhamu’
Mimi nimewahi kutupiwa pesa niliyokuwa nimemlipa Master J kwa ajili ya kurekodi ngoma yangu ‘Mwanangu Huna Nidhamu’,” alisema Dudu.
“Ilikuwa elfu 15 na Master J alikuwa amenipangia kwenda kurekodi Jumamosi lakini ilikuwa kila ninapoenda ananiambia niko bize njo Jumamosi ijayo.
“Nilienda kama Jumamosi sita 6 bila kurekodi. Mwisho wake tulipishana kauli na akanitupia mkwanja wangu. Enzi hizo mwaka 2000, Master J alikuwa anawapenda sana 2proud a.k.a Mr 2 na kundi la Diplomatiz la Saigon na Dollaso pamoja na Kwanza Unit.” Alifafanua Dudu.
Aliongeza, “Tabia hii ipo dunia nzima kwa producer kupenda msanii au wasanii flani. Si kuwa na kinyongo na Master J kwa sababu najua unaweza kukataliwa na producer au lebo flani kwa sababu amekusikiliza akiwa katika mood mbaya au kiwango chako kipo chini.
“Mwanangu Huna Nidhamu nilifanya beat na Maron Minje hapo hapo MJ Rec na vocal nikaenda TMK kwa Enrico ndipo ngoma ikatoka na ikahit na mimi nikawa star.
“Mwaka 2001 ndipo urafiki na Master J ukaanza, mimi nikawa ndiye star wa MJ Rec ndiye producer aliye produce album yote ya amri 10 za mungu, Lakini yote niliyopitia sikuweka kinyongo na mtu, nilijua haya ni maisha tu,”
Pia, Dudu Baya baada ya kufanya poa na kuanzisha label yake ya Dar Skendo, amedai alimkataa Mr Blue baada ya kuona hana kipaji.
“Nimewahi kumkataa Mr Blue nikiwa na lebo yangu ya Dar Skendo. Mr Blue alikuja na single yake ya ‘Blue Blue’. Sikuiona kama ni ngoma kali. Wakati huo mapenzi yangu yote yalikuwa kwa Dogo Hamidu. Lakini Mr Blue hakukata tamaa, alienda G. Recordz na akapokelewa na akatusua na ngoma hiyo.
“Namchompendea Mr Blue hakuonyesha kinyongo kwangu na tuliendelee kuwa pamoja na yeye kuwa karibu na Dogo Hamidu mpaka leo, na hakuna msanii mwenye heshima na anayejitambua kama Mr Blue ndio maana mpaka leo yupo kwa hewa,” alisema Dudu.