Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dudu Baya afunguka gonjwa la ajabu linalomsumbua

Dudubaya Dudu Baya afunguka gonjwa la ajabu linalomsumbua

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini 'Dudu Baya' amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu maradhi ya ajabu yaliyomkumba ambayo yanamsumbua tangu mwaka 2021.

Dudu Baya amesema kuwa Miguu yake ilikosa nguvu na mwili mzima alikuwa hawezi kusimama hata haja kubwa na ndogo alikuwa hawezi kwenda.Dudu baya anasema hawezi kuacha Harakati za kupigania maslahi ya wasanii wasio na nguvu ambao wananyonywa na wenye nguvu.

Dudu Baya amesema kuwa wasanii wengi sana wa Bongo Fleva wanaishi maisha kwenye vifungo vya maisha na ndio maana wengi wao wameingia kwenye maisha ya kutumia madawa ya kulevya kwa sababu ya mawazo.

Ameongeza kuwa msanii pekee Tanzania anayeishi maisha ya amani na ya furaha ni Alalikiba huku akidai kuwa wasanii wengi wananyanyasika sana licha ya kuonekana wakipost magari ya gharama na majumba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live