Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dudu Baya: Hakuna Msukuma 'chawa', wengi wanatoka Kigoma

Dudubaya Na H Baba Dudu Baya

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa HipHop Bongo, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya au Mamba 'Konki Master' amesema kuwa hakuna mtu kutoka kabila lake la Kisukuma ambaye anaweza kufanya kazi ya 'uchawa' kwa kumsifia mwanadamu mwenzake.

Dudu Baya amesema hayo wakati akiwazungumzia baada ya mastaa Bongo kugeuka kuwa machwawa kwa mastaa wengine ili tu waweze kuishi mjini.

“Niliwahi kuwa na Wasafi lakini sikuwa kama chawa, ila yeye kwa vile kajiweka kama chawa basi aendelee kumsifia Diamond. Kwa sababu haya maisha unaamua mwenyewe, hata H.Baba alikuwa akimsifia harmonize na kumponda Diamond, baada ya hapo akaenda tena kwa Diamond.

“Mwijaku na Baba Levo wamechagua kuwa chawa, lakini ukitaka kuwa Konki basi uwe Konki kama Konki Master. Mimi siwezi kuwa chawa kwenye maisha yangu. Hakunaga Msukuma chaw ahata siku moja, machawa wengi wanatokea Kigoma.

“Tazama Mwijaku Kigoma, Baba Levo Kigoma, H.Baba Kigoma, ukija Juma Lokole Kigoma kwa hiyo machawa wote wanatoka kule, ni hulka zao. Watu wa Kigoma wengi ni Wamanyema na wale wanatokea Congo DR.

“Wacongo wanapenda kusifia sifia, angalia hata Wacongo waliopo Dar, kujioendekeza hata kumtungia mtu wimbo,” amesema Dudu Baya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live