Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dua ya Kajala noma, kumnunulia Paula Range mbili

Paula Na Mama Yake Kajala Dua ya Kajala noma, kumnunulia Paula Range mbili

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kajala Masanja aka Mrs Harmonize mtarajiwa anaendelea kuchukua vichwa vya habari katika ulimwengu wa burudani ambapo safari hii, amefanya Dua ya kupata kununua gari aina ya Range mbili kwa ajili ya mwanaye kipenzi, Paula.

Mpango mzima umejiri usiku wa kuamkia leo Julai 23, 2022 alipokuwa akisherehekea bethidei yake pamoja na watu wake wa karibu.

Kwenye kipande cha video ambacho kimevuja mitandaoni, Kajala anasikika akikata keki na watu wake wakimuimbia na ndio alipotoa Dua hiyo.

"Ee Mwenyezi Mungu unijalie niweze kufika mwakani, unijalie niweze kumnunulia mwanangu Paula Range mbili," alisikika Kajala huku akikata keki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live