Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dr. Cheni awapongeza Nandy na Billnass kwa kupata mtoto

NANDY BILLNASS PUNDAZ Dr. Cheni awapongeza Nandy na Billnass kwa kupata mtoto

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

habari njema kutoka kwa mastaa wa Bongo Fleva, bwana na bibi harusi wapya mjini, Nandy na Billnass ambao wamefanikiwa kupata mtoto baada ya Nandy kujifungua.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mshereheshaji 'MC' Dr. Cheni aliyeendesha shughuli ya harusi yao iliyofanyika mwezi uliopita jijini Dar.

Dr. Cheni ameyaeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram bila kutaja jinsia ya mtoto huku akiambatanisha picha ya siku ya harusi ya Nandy na Billinas kwa kuandika kuwa;

“Woow congratulations Mr and Mrs Billnass na Nandy kwa kupata mtoto, Mungu awalindie kitoto chenu, mbarikiwe sana,” ameandika Dr Cheni.

Hata hivyo, wawili hao (Nandy na Billnass) hawathibitisha kama habari hizo ni za ukweli au la.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live