Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dr Almasi ajifananisha na Diddy, R Kelly na Snoop

Polish 20240520 104924276 Dr Almasi ajifananisha na Diddy, R Kelly na Snoop

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuzeeka ni mpango wa Mungu ila kuchoka ni kujitakia kauli hii ameitoa Mwigizaji Steven Charles Almasi maarufu kama DrAlmasi baada kuzungumza.

“Mimi nina watoto na wajukuu lakini sijaruhusu kuchoka bado najikubali kutokana na mtindo wangu wa maisha kwa sababu ukiangalia katika jamii yetu wazee wengi wamejichagulia kuchoka na kuchakaa sasa mimi kwangu ni tofauti sijachagua kuchakaa.

“Walio wengi wanaamini ukiwa mzee au umri umeenda basi hutakiwi kuvaa vizuri, kujipulizia pafyume na kwenda na dunia inavyoenda hususani kwa zama za sasa” Amesema.

Kutokana na mwonekano wake amesema unampatia deal nyingi za mambo ya fashion huku akidai kuwa anawatazama zaidi Snoop Dogg, P Diddy, R Kelly

“Watu wanatakiwa wajue mimi siishi katika mipaka ya Tanzania au life style ya hapa kwa sababu mimi ni fashionist ambaye naangalia mitindo na mionekano kutoka njee hususa kwa wasanii wenye umri kama wa kwangu ambao tumeachana miaka miwili au mitatu kama akina #SnoopDogg, #PDiddy, #RKelly” Anasema Dr. Alimasi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live