Muigizaji wa Bongo Movie, ambaye alijulikana zaidi kupitia tamthilia ya ‘Jua Kali’ Dorah ameeleza kuwa anachukizwa na watu wanaosema kuwa hawezi kuwa na Mahusiano kwa sababu ya kuonewa huruma jinsi alivyo.
Dorah ameyasema hayo akiwa katika mahojiano na mmoja ya chombo cha habari ambapo ameeleza hisia zake na kuwaonya watu wanaoendelea kumsema hawezi kuwa na mpenzi huku akiwataka waache mara moja kwani hajisikiii vizuri kuona baadhi ya watu kumuona ni mtu wa tofauti na wengine.
Hata hivyo, ameweka wazi kuwa yeye ana mpenzi na mahusiano yake ni ya muda mrefu lakini hawezi kum-post mpenzi wake katika mindao ya kijamii kwa sababu ni maisha yake private hivyo haina haja kila mtu kuyajua. .